HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 25, 2016

NAIBU WAZIRI, ANASTAZIA WAMBURA ALITEMBELEA MAKAO MAKUU YA STARTIMES BEIJING NCHINI CHINA.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) na  Rais wa  kampuni ya kimataifa ya StarTimes Pang Xinxing (kushoto). Mhe. Naibu Waziri alitembelea studio za StarTimes  zilizopo mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hizo.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania na kampuni ya StarTimes  walipotembelea studio za StarMedia zilizopo mjini Beijing nchini China leo kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa akifuatiwa na Erick Xue, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang    akifuatiwa na Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya  nchi za nje wa StarTimes William Lan.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akifanya mahojiano na mtangazaji wa StarTimes ambaye ni Mtanzania David (kushoto) wakati alipotembelea studio hizo leo  zilizopo mjini Beijing nchini China kwa ajili ya kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na studio hizo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Picha na mpigapicha wetu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad