HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2016

KUMEKUCHA UWANJA WA TAIFA, NI BAADA YA KUTANGAZIWA KUINGIA BURE

Kufuatia Uongozi wa Klabu ya Yanga kuwatangazia washabiki wao kwamba Mechi ya Timu yao dhidi ya TP Mazembe ya Nchini Congo inayopigwa leo katika dimba la Taifa, kuwa haitakuwa na viingilio, Mapema asubuhi hii Mashabiki hao wamejitokeza kwa wingi na kupanga foleni katika mageti yote ya kuingilia uwanjani hapo kusubiria kuanza kwa utaratibu wa kuingia uwanjani hapo kwa lengo moja la kuipa nguvu timu yao, inayoshiriki katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho. Ripota wa Globu ya Jamii ambaye yupo Uwanja wa Taif hivi sasa, anaeleza kuwa Mashabiki hao walianza kujitokeza kuanzia saa 12 asubuhi, huku wengine wakisema kuwa wameamua kuja mapema ili kuujaza uwanja na kutowapa nafasi watani wao ambao inadaiwa kuwa walisema wataiunga mkono hiyo timu ya kigeni.
 Hapa mageti yakifunguliwa tu, watu ndani.
 Msururu wa Washabiki wa Yanga nje ya Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad