HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2016

WANACHAMA WA YANGA WASUASUA UCHAGUZI MKUU.

Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii.
KATIKA kuelekea uchaguzi Mkuu wa Yanga na dirisha la kuchukua fomu kufunguliwa siku ya Ijumaa na linatarajiwa kufungwa kesho Juni 01 inasadikiwa hakuna mtu yoyote ameyejitokeza tayari kuchukua fomu huku Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TFF,Aloyce Komba akiwa nje ya mji na anatarajiwa kurejea kesho.

Baadhi ya wanachama wa Yanga wameonesha kutokuelewa uchaguzi kama utafanyika kwani hakuonekani dalili za kuelekea uchaguzi hu Juni 25 na zaidi wanashangaa Shirikisho la Mpira 

wa Miguu (TFF ) ndilo linalohusika na utoaji huo wa fomu na kama serikali wameamua iwe hivyo sawa.

Akitolea ufafanuzi wa uchaguzi, Katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdesit amesema wao wameamrishwa kufanya uchaguzi na serikali na tarehe imeshapangwa watafanya kama walivyoelekezwa zaidi masuala mengine yote anatakiwa kujibu mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi TFF,Aloyce Komba ila wao kwa sasa wapo kwenye majadiliano juu ya kadi za kutumika kwenye uchaguzi huo kati ya za zamani na mpya.

"Suala la uchaguzi hatuwezi kuliongelea sisi tupo kwenye majadiliano ya kadi za kutumika kwenye uchaguzi huo wa Juni 25 na zaidi sisi viongozi wa Yanga ndiyo tunaowajua wanachama wetu na wanavyotaka kusema kuwa tutumie kadi za zamani basi hakuna hata mwanachama mmoja atakayepiga kura kwani toka 2014 hakuna hata mmoja aliyelipia kadi za zamani,"amesema Deusdedit.

Tutatoa tamko baada ya kuhusiana na kadi gani zitatumika siku ya uchaguzi ila wanachama wavute subira kwani sisi tunawatambua kama ni wanachama wetu na watapiga kura.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad