HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 27, 2016

VETA YAWAPA MAENDELEO YA MRADI WA WANAGENZI (DUAL APPREATICESHIP) WADAU WA VIWANDA.

MAMALAKA ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA) ikishirikiana na wadau kutoka viwanda vya umeme na umeme wa magari wametoa maendeleo ya mradi huo kwa wadau wa viwanda.

Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko wakati akizungumza na wadau wa viwanda vya umeme na umeme wa magari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa mafunzo hayo yanaumhimu mkuwa kwa viwanda kwani mafunzo hutolewa kwa umahili mkubwa kwa walichaguliwa kujifunza mafunzo hayo kutokana na mahitaji ya kiwanda.

Bukko amesema kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya vitendo zaidi (Hands & Skills) chini ya Mradi wa ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman.

Amesema kuwa utaratibu wa mafunzo hayo yamaendaliwa kutoka na vyuo vya mafunzo ya ufundi Stadi.
Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko akizungumza katika mkusanyiko wa wafanyakazi,viongozi wa Veta pamoja na (Wanagenzi) wanafunzi wanafanya mafunzo yao katika viwanda mbalimbali hapa nchini waliojiunga katika mradi wa wanagnizi(APPREUTICESHIP) jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa mradi huo unawajulisha wanafunzi wanataka kujiunga na mafunzo hayo katika chuo cha Veta na kufanya kazi katika viwanda mbalimbali hapa nchini kuwa mafunzo hayo hayana gharama yoyote na unajifunza katika kiwanda unachohitaji kutokana na taaluma yako.

Baadi ya wadau wa Veta wakimsikiliza Mkurugenzi wa kanda ya Dar es Saalam, Habibu Bukko jijini Dar es Salaam leo.

Meneja wa Mradi wa Appreaticeship kutoka kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman, Maltin Mac Mahon akizungumza na wadau wa Veta jijini Dar es Salaam leo na akielezea jinsi alivyowafundisha wanafunzi wa veta ambao wapo na ambao hawapo viwandani hapa nchini kutengeneza vitu vya umeme pamoja na umeme wa magari hapa nchini pamoja na vitu mbalimbali vilivyopo katika viwanda mbalimbali kutokana na mahitaji ya kiwanda husika.
Wadau wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mradi wa Appreaticeship kutoka kampuni ya Handwerkammer Humbarg ya Ujeruman, Maltin Mac Mahon (Mbele) jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapa maendeleo ya mradi wa wanagenzi.(Appreaticeship).
Baadhi ya wadau wakisikiliza maada katika mkutano wa kuwapa maendeleo ya mradi wa wanagenzi (Appreaceship) jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wanafanya mafunzo katika viwanda mbalimbali hapa nchini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo cha mafunzo ya ufundi (VETA) jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad