HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2016

UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MARA

UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa naShirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Musoma mkoani Mara siku ya Jumanne na Jumatano, Mei 31-Juni 1, 2016. Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
 
PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Magesa Mulongo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah.

Watu takribani 200 walihudhuria. Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Mara, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.

Mkoa wa Mara una Halmashauri tisa, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Mji wa Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.

Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Ally Maftah akizindua mradi wa Uboreshaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3 Mkoani Mara leo. Maftah alizindua mradi huo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. PS3 inatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara kupitia Halamshauri 97 chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Mtaalam wa Fedha wa mradi huo, Abdul Kitula akizungumza ambapo alisema kuwa PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.

Kaimu Katiobu Tawala Mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akizungumza.
Baadhi ya washiriki ambao ni Wakurugenzi na watendaji wengine kutoka Mara wakifuatilia uzinduzi huo.

Picha ya pamoja na washiriki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad