HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 25, 2016

SIMBA YATAKIWA KUSAJILI WACHEZAJI WAZURI NA SIO MAJINA- MGOSI.


Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
MSHAMBULIAJI wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi(Pichani) amesema, kuelekea katika usajili wa wachezaji wapya viongozi wanaqtakiwa kuangalia ambao wanahaki ya kuitetea simba na sio kusajili mchezaji kwa sababu ya jina lake.

Mgosi amesema, Klabu inatakiwa kusajili wachezaji ambao wataipa Simba kile kitu ambacho kinakihitajika ili kuiweka timu katika nafasi nzuri.

Mgosi amesema, wachezaji wa kigeni wanahitajika lakini waangaliwe kama ni watu aina gani wanahitajika na wanauwezo wa kuitetea timu kwa kazi watakayoifanya.

"Mchezaji wa kigeni anatakiwa kufanya kazi ya ziada ambayo itamzidi yule mchezaji mzawa ili kuweza kuweka utofauti kati ya mchezaji wa kimataifa na mzawa katika klabu,"amesema Mgosi. Hilo limekuja baada ya wachezaji wa kigeni wa timu hiyo kucheza chini ya kiwango ukilinganisha na wazawa na wengine kuishia kuishia kukaa benchi.

Mgosi amesema, viongozi wanatakiwa kuangalia makosa yaliyotokea katika msimu uliopita na kupelekea timu kushindwa kufikia malengo ili kuyarekebisha na hata usajili utakapofanyika uwe wa kueleweka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad