HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2016

PST KUTOKUJIHUSISHA NA NGUMI HADI 2019.

Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
SERIKALI kupitia Baraza la Michezo (BMT) limefungia Shirikisho la mchezo wa Ngumi za Kulipwa nchini (PST) kujihusisha na ngumi hadi kuanzia jana Mei 31 hadi Mei 2019, PST wameshushiwa rungu hilo baada ya kuchezesha watoto wenye umri chini ya miaka  10 na kumuajiri mnadi miunguko(Card Girl) mtoto mwenye umri chini ya miaka nane kinyume na sheria.

Mbali na kufungiwa kwa shirikisho hilo pia Serikali imesitisha uteuzi wa PST, Emmanuel Mlundwa kama mjumbe wa kamati ya kutengeneza katiba, kanuni na taratibu za kufuatwa katika michezo ya ngumi za kulipwa.

Akitoa tamko hilo Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa Katika pambano lililofanyika Mei 14 kati ya Thomas Mashali na bondia wa Iran, Sadjadi Meherab waliwachezesha watoto hao huku kitendo kama hicho pia kikiwahi kutokea Juni 18 mwaka 2002. "Katika pambano hilo PST walimtumia mtoto Joyce Francis ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kama mnadi mizunguko katika pambano hilo", amesema Kiganja.

Amesema kuwa Mlundwa na katibu wake Anthony Rutta hawatapewa kibali chochote na serikali cha kuratibu mapambano hayo ndani wala nje ya nchi.

"Tumewafungia kina Mlundwa kuanzia leo hivyo mialiko yote ya mabondia itapitia mezani kwangu na kamati itayashughulikia bila kuathiri haki za mabondia na hao washiriki katika mashindano", amesema Kiganja. Baada ya kusikiliza utetezi wa Mlundwa juu ya suala hilo  PST wamesema wapo tayari kusitisha mapambano ya watoto ikiwa ni maoni kama kusitisha huko kutazorotesha maendeleo ya mchezo huo.

Amesema kuwa BMT walitegemea kukuta utetezi wake utataja mamlaka yaliyomruhusu kuandaa ngumi za watoto lakini kwa bahati mbaya hawakukutana na kipengele hicho katika utetezi wake kutokana na suala hilo Serikali imevitaka vyama vyote vya michezo kuheshimu na kuepuka kufanya kazi bila kufuata kanuni za mchezo husika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad