HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 2, 2016

RC MAKONDA AWASAINISHA MKATABA WA WIKI MOJA WAKUU WA IDARA KUSAKA WATUMISHI HEWA

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugeni pamoja na wakuu wa idara mabalimbali za manispaa na jiji la Dar es Salaam leo.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakiapa kiapo cha mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jijini la Dar es Salaam leo walipo apishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakisaini mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa zao jijini Dar es Salaam, na atakaye shindwa kuwajibika  katika kufanya kazi  na baadae wakija kujulikana atawajibishwa yeye.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa mkataba wa wiki moja wakuu wa Idara za Manispaa za jiji la Dar es Salaam kutafuta watumishi hewa.

Wakuu wa Idara za Manispaa watakaoshindwa kufanya hivyo wataundiwa tume ambayo itapita katika manispaa hizo kuhakiki watumishi hewa na endapo watumishi hewa wakibainika kuwepo mzigo utabebwa na wakuu wa Idara kulipa mishahara hewa hiyo.

Makonda ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Pamoja na Wakuu Idara mbalimba za manispaa za jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa mkataba huo kila mtu lazima afanye kazi  na sio  na  kukimbizana au kuamrishishana.

 Amesema kuwa mara ya kwanza walipatikana watumishi 71 lakini baada ya kuweka mkazo wamefikia 209 ambao wanalipwa zaidi ya sh.bilioni 2.9 ambapo fedha hiyo zingefanya kazi nyingine ya kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa kusukumana wakati kazi hiyo waliomba wenyewe na kuahidi kutekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa kwenda kuangalia vitu vya kihuduma kwa wananchi sio yake, lakini inatokana na wale wenye wajibu wa  kutekeleza majukumu yao kufanya uzembe tu.

 Makonda amesema kuwa zoezi la kutafuata watumishi hewa lazima lifike kikomo na kuweza kufanya mambo mengine ya kutatua changamoto za wananchi ambazo zimetokana na watu kujisahau kutimiza wajibu wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad