HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 29, 2016

MKAKATI MPYA WA KITAIFA WA KUPANDA NA KUTUNZA MITI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mbarak Abdulwakil (kushoto) akifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na MazingiraNgosi Mwihava.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
SERIKALI imeandaa mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda na kutunza miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hatua ambayo itarudisha hali ya mazingira kama yalivyokuwa awali miaka ya nyuma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.

 “Mkakati huu mpya umezingatia kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika kampeni za upandaji miti zilizofanyika katika vipindi mbalimbali tangu uhuru wan chi yetu” alisema Waziri Makamba.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Makamba amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imetenga kiasi cha Sh. bilioni 2 ikiwa kianzio kwa lengo la kusimamia mkakati huo katika mwaka wa fedha 2016/2017. 

Katika kuhakikisha suala la mazingira limepewa kipaumbele, Mfuko wa Taifa wa Mazingira ambao ni mdau mkuu wa mazingira utatengewa vyanzo vya mapato yanayokadiriwa kufikia Sh. bilioni 100 ikiwa ni juhudi za kugharimia mpango huo na mipango mingine ya hifadhi ya mazingira.

Mkakati huo ni wa miaka mitano ambao unaanza kutekelezwa 2016 hadi 2021 na unakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 105.2. 

Aidha, Waziri Makamba amebainisha kuwa masuala ambayo yatazingatiwa katika kutekeleza mpango huo ni pamoja na uhamasishaji na utoaji motisha kwa watumiaji wa nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa.

Ili kuhakikisha mazingira yameboreshwa na yawe rafiki kwa kila kiumbe, utekelezaji na usimamiaji wa mkakati huo, utaanza kutekelezwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu ambapo kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya na kila taasisi itapewa lengo la pandaji miti kama msingi wa zoezi hilo.

“Tutashindanisha shule na vijiji katika upandaji na ukuzaji wa miti na tutatoa zawadi nono na maeneo ya wazi ya Serikali yatapandwa miti” alisema Waziri Makamba.

Katika kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kukua,  Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha halmashauri zinatunga sheria ndogo ndogo za kuhimiza upandaji na utunzaji miti nchini.

Maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa yanafanyika nchini Angola ambayo yanalenga kupambana na biashara ya meno ya tembo na pembe za faru yakiongozwa na kaulimbiu “Tunza wanyama porini kwa maisha”
Siku ya mazingira Duniani imeanza kuadhimishwa  mwaka 1972 ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa lilifanya wa mkutano wake wa kwanza unaohusu mazingira uliofanyika Stockholm nchini Sweden na kuundwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira diniani (UNEP).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad