HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2016

Meli tatu za Jeshi la maji kutoka China zawasili Bandari ya Dar es Salaam

Meli tatu za Jeshi la maji kutoka China zilifika katika Bandari ya Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kuendeleza na kuboresh ushirikiano wa nchi hizi katika eneo la majeshi ya majini ulioanza miaka ya 1960.

Meli hizo zilizotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa zinatarajiwa kuwa hapa nchini kwa siku nne, kuanzi jana ambapo majeshi ya maji ya nchi hizi mbili yatafanya mazungumzo kubalishana uzoefu na mafunzo.

Meli hizo zilipokelewa na Balozi wa China nchini Tanzania, Dk Lu Youqing, Mkuu wa Tawi la Mipango na Mendeleo Jeshini, Meja Jenerali Simon Mumwi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania na Mkuu wa Jeshi na Maji nchini Tanzania Meja Generali Rogastian Shaaban Laswai. Maofisa wa Jeshi na Balozi waliikagua moja ya meli za kivita zilizofika nchini, meli hilo iliidhinishwa kuanza kufanya kazi mwaka jana.

Dr Youqing alisema ujio wa meli hizo ambazo zitakuwa nchini kwa siku nne utaboresha zaidi ushirikiano katika eneo la Jeshi la maji kati ya nchi hizi mbili. “Tukio hili litatoa fursa nzuri kwa nchi hizi kubadilisha uzoefu na mafunzo kama sehemu ya ushirikiano,” alisema.

Meja Generali Mumwi alisema ujio wa meli hizo ni fursa kwa Tanzania kuzungumza na Jeshi la Maji la China ili kujua namna ya kukuza ushirikiano ambao utaisadia Tanzania kufikia lengo lake la kuleta mabadiliko katika majeshi yake. “Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuliboresha Jeshi letu ili liwe na vifaa vya kisasa na kufanya Mapinduzi ili kukidhi mahitaji ya usalama kwa sasa,” alisema Mumwi.

Alisema China inaweza kuisaidia Tanzania katika kufikia lengo hili kwa kutoa mafunzo na msaada unaohitajika kuleta mageuzi katika Jeshi la Kujenga Taifa. Alisema Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania linahitaji mafunzo, vyenzo za kisasa na mambo mengine yatakayoliwezesha kukidhi mahitaji ya sasa.

Mkuu wa Jeshi la Maji nchini, Laswai alisema siku nne za ujio wa meli za kivita kutoka China zitatumika katika kujadili mipango mbalimbali kwa manufaa ya Tanzania na China. “Kesho (leo) tutakuwa na mazungumzo katika makao makuu ya Jeshi la Maji la Tanzania ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa kwa undani zaidi,:”alisema Laswai.
Mkuu wa Jeshi la Maji nchini Tanzania, Meja Jenerali, Rogastian Shaaban Laswai akitoa heshima za kijeshi kwa Jeshi la maji toka China mara baada ya Meli za Kivita kutoka China kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam jana.
Kutoka kulia: Kiongozi wa Meli va Kivita toka China, Chen Qiang Nan, Mkuu wa Jeshi la Maji nchini Tanzania, Meja Jenerali, Rogastian Shaaban Laswai, Balozi wa China nchini Tanzania, Dk Lu Youqing na Mkuu wa Tawi la Mipango na Mendeleo Jeshini, Meja Jenerali Simon Mumwi wakipata Maelezo kuhusu meli za kivita toka China, jana katika Bandari ya Dar es Salaam. Picha/ Ubalozi wa China

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad