HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 6, 2016

MCHEZO WA KUCHEZWA NCHINI KENYA NA TIMU YA TAIFA.


 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo, Ismail Bura (kulia) akionesha Kocha Mkuu wa mchezo wa Roll, Aurher Haule sampuli ya sare za Taifa zinazofaa kuvaliwa na wachezaji wanapokuwa nje ya nchi.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty ,Nadia Azmat akimkabidhi jezi kocha Mkuuwa timu ya Taifaya Tanzania ya mchezo waRoll, Aurther Haule  zitakazotumika kuchezea mchezo wa Roll kwa nchi zaAfrika utakakaofanyika Kenya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty ,Nadia Azmat akionesha viatu vitakavyotumika kuchezea mchezo wa Roll kwa nchi zaAfrika utakakaofanyika Kenya.

Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Taifa ya Mchezo wa mpira wa kuteleza(Roll Ball) imeondoka jana ikiwa na wachezaji 12 kwenda Kenya kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayoanza leo mjini Nairobi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Arthur Haule alisema jana Dar es Salaam kuwa wamejiandaa kutwaa ubingwa wa mchezo huo utakaoshirikisha timu kutoka mikoa sita.

Alisema safari yao ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Nadia House of Beuty inaondoka na wachezaji 12 na viongozi wawili.

Aliwataja wachezaji watakaowakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Mohammed Athumani, Emmanuel Thomas, Hamisi Salum, Rajab Kassim, Omari Madohola, Yakhe Shaaban,Jonas Emmanuel, Fahadi Waziri, Said Abdallah,Kassim Rajab, Feruzi Juma na Clement Andrea.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia House of Beuty, Nadia Azmat akikabidhi vifaa vya michezo kwa safari hiyo aliwataka watanzania wengine kusadia michezo ambayo haina umaarufu ili kuibua vipaji mbalimbali vya vijana.

Nchi zinazoshiriki mashindanoi hayo ni wenyeji Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad