HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 25, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA: YANGA YATWAA KOMBE LA SHIRIKISHO LEO, YAICHAPA AZAM FC BAO 3-1 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

 Rais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub, mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1, katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es salaam. Picha na Othman Michuzi.
 Wachezaji wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia bao la kuongoza aliloipatia timu yake dhidi ya Azam FC , katika mchezo uliopigwa jioni hii, ikiwa ni mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1. Picha na Othman Michuzi.
Kiungo Mshambuliaji wa timu ya Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" akiichambua ngome ya Timu ya Yanga, katika mchezo uliopigwa jioni hii, ikiwa ni mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1.
 Mchezaji wa timu ya Yanga Oscar Joshua akimzuia mchezaji wa timu ya Azam FC Himid Mao kwenye mchezo wao wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Shirikisho (ASFA) ulichezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wametwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC baao 3-1.
Lango la Azam  FC likiwa hatarini kuvunjwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad