HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2016

MASHINDANO YA VIJANA CHINI YA MIAKA17 YA MPIRA WA MIGUU KUANDALIWA NA ILALA.

Mwenyekiti wa chama cha Mpira  wa Miguu vijana  Ilala Faza Edwin Mloka akizungumza Globu ya Jamii jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
MWENYEKITI wa chama cha Mpira  wa Miguu vijana  Ilala Faza Edwin Mloka wapo kwenye mikakati ya kuandaa mashindano ya vijana ya chini ya miaka 17 na timu zote za manispaa hiyo zitakutana kesho katika ofisi za chama cha mkoa Dar es salaam DRFA na zaidi wanatakiwa kufika walimu pamoja  na katibu mkuu wa timu.

Mloka amesema, wao kama viongozi wa mpira hususani katika kuendeleza soka la vijana wanataka vijana wadogo walio na umri wa miaka 16 na kushuka chini na katika mashindano hayo watatumia fursa kuweza kupata wachezaji wa baadae watakaoleta changamoto baadae.

"Unajua vijana ndiyo watakaoleta chamgamoto katika soka la kesho,kwahiyo katika mashindano hayo tutahitaji vijana walio na umri chini ya miaka 16 ili kuweza kuwajenga katika misingi ya kimpira,"amesema Mloka.

Katika mashindano hayo pia watatumia nafasi ya kutafuta timu ya wilaya itakayokuja kutumika hadi kushiriki michuano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad