HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2016

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO BAADA YA KUANZA RASMI KWA MABASI YAENDAYO HARAKA JIJINI DAR

 Yale mabasi yaendayo haraka, tuliyokuwa tukiyasubiri kwa hamu kwa kipindi kirefu, hatimae leo yameanza kazi rasmi kwa ruti zote zilizopangiwa. pamoja na kuanza kwa kazi, lakini bado wanachangamoto ya matumizi ya njia yake, kwani bado kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vimekuwa vikiitumia njia yake hiyo kana kwamba ni jambo la kawaida tu. Leo Kamera ya Mtaa kwa Mtaa imezungukia eneo la Kariakoo na kujioneka hali halisi katika barabara hiyo na kukuletea wewe mdau ujionee mwenyewe na kutoa maoni yako ya nini kifanyike ili jambo hili likae kwenye mstari ulionyooka. Picha na Emmanuel Massaka.
 Ile kuchomoza tu, nakutana na Daladala hili likiwa limeifunga kabisa njia hiyo kwa lengo la kukatisha barabara hiyo kurudi lilikotoka baada ya kuona chombo chenye njia yake kikichomoza mbele yake.
 Bodaboda na Watembea kwa miguu wakijidai katika barabara hiyo.
 Yaani mwendo wa madaha kwa kwenda mbele.
 Hawa nao ndio kama wanavyoonekana.
 Kupishana.
 Abiria wakisubiri mabasi hayo kwenye moja ya kituo.
Abiria ndani ya basi.

5 comments:

  1. Yani Watanzania ustaarabu ni 0 Kabisa... Kwanini wasikamatwe tu na adhabu kali sana.

    ReplyDelete
  2. Kuwalazimisha kuheshimu sheria kwa askari trafiki kuwatoza faini kubwa sio elfu 30. awe bodaboda au gari au mkokoteni baiskeli wote watozwe elf 50 kwa kila kosa. bada ya muda mfupi hawata tumia hiyo barabara tena.
    Jamani waTanzania wa gumu kuelewa na kushika sharia.

    ReplyDelete
  3. Kwa maoni yangu hii sio sawa kabisa ilibidi serikali iweke kzuizi ili hizo barabara zitumiwe na mabasi hayo peke yake kwa sababu sisi wabongo ni wabishi ,hatujali na hatupendi kufuata sheria hilo jambo litatugharimu sana

    ReplyDelete
  4. Yani Watanzania ustaarabu ni 0 Kabisa... Kwanini wasikamatwe tu na adhabu kali sana.

    ReplyDelete
  5. Kwa maoni yangu hii sio sawa ilibidi serikali iweke kizuizi ili hizo bara bara zitumike na mabasi hayo tu, kwa sababu sisi wabongo ni wabishi ,hatujali na hatupendi kufuata sheria hilo jambo litatugharimu sana

    ReplyDelete

Post Bottom Ad