HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 28, 2016

Godown lanusurika kuteketea kwa Moto jijini Dar leo

 Godawn la Kampuni ya Simba Mtoto lilolopo eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es salaam, limenusurika kuteketea kwa moto usiku huu, baada ya vijana wawili waliokuwa wakiishi katika eneo lilolopo jirani na hapo, kuchoma matairi mabovu yaliyokuwepo ndani ya eneo lao hilo. Walipoulizwa zababu za wao kufanya hivyo, vijana hao waliofahamika kwa majina ya Peter na Amdan, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi, walisema kuwa walifanya hivyo kwa lengo la kupunguza wingi wa majani yaliyolizunguka eneo hilo na hawakuwaza kama moto huo ungeshika kwenye matairi hayo ambayo ni chakavu ya magari yaliyokuwamo ndani ya eneo hilo. Taharuki ilitanda eneo lote la Tabata pale moshi mwingi na mzito ulipotanda angani na kuwafanya hata wale waliokuwa kwenye mapumziko ya mwisho wa wiki kushindwa kufanya hivyo huku wengine wakifanya mawasiliano na baadhi ya ndugu zao waliowaacha majumbani. Hadi Ripota wetu anaingia mitamboni hakukuwa na madhara yeyote yaliyotokea na jitihada za kukitafuta kikosi cha Zimamoto na Uokoaji zilikuwa zikiendelea. Na vijana hao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi. 
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka.
vijana hao ambao walifahamika kwa jina Moja Moja, Peter na Amdan wakipakizwa kwenye gari ya Polisi.
Vijana hao wakiwa chini ya Ulinzi. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad