HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 31, 2016

Dar Brew yazindua muonekano mpya wa Chibuku Super

KAMPUNI ya Dar Brew, imezindua chupa mpya ya bia ya asili ya Chibuku Super yenye ujazo wa mililita 750, ambayo mtumiaji halazimiki kurudisha chupa pale anapoitumia.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa Dar Brew, Oscar Shelukindo alisema, bia hiyo iliyopo katika chupa nzuri ya plastiki inayovutia, itauzwa kwa bei ya Sh 1,000 tu kwa kila chupa.
“Bia hii imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo tunawahakikishia watumiaji ubora wa hali ya juu,” alisema.

Shelukindo alisema, bia hiyo imetengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mtama ulio bora, hivyo kuna kila  sababu kwa Watanzania kujivunia kilicho chao na kukumbuka asili yao, kwani hii ni bia yao ya asili.

Naye Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo alisema, bia hiyo itaanza kupatikana nchi nzima katika baa, maduka makubwa (Super Markets), katika maduka ya jumla na rejareja na sehemu zinazouzwa vileo kuanzia leo.

Kazindogo alisema, ana imani kubwa wapenzi wa bia wataipokea kwa shangwe na wataitumia ili kuonesha wanajali asili yao.
Meneja Masoko wa Dar Brew, Oscar Shelukindo akizungumza wakati wa kuzindua chupa mpya ya bia ya asili ya Chibuku Super yenye ujazo wa mililita 750, jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo akifafanua jambo juu ya ujazo wa chupa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad