HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 27, 2016

AZAM MEDIA YASAINI MKATABA WA BILION MBILI KURUSHA LIGI YA WANAWAKE NA U20.


 Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington wakisaini Mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni mbili kwaajili ya kurusha matango ya Mojakwa moja ya Ligi ya wanawake na vijana wa chini ya miaka 20.
 Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) akizungumza kabla ya kusaini mkataba kati ya TFF na Azam Media kwaajili ya kurusha matangazo ya mpira wa Miguu, Ligi ya Wanawake Taifa na Ligi ya Vijana wa chini ya miaka 20. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington.
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), Jamal Malinzi,(Kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ryhs Torrington wakibadilishana mikataba jijini Dar es Salaam leo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Nchini (TFF) limeingia mkataba na kampuni ya Azam Media wenye thamani ya Bilioni 2 kwa muda wa miaka mitano ikiwa ni kwa ajili ya kurusha matangazo ya ligi kuu ya wanawake pamoja na ligi ya vijana U-20 itakayoanza mwezi August mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Raisi wa TFF, Jamal Malinzi amesema kuwa mkataba huo ni wa miaka mitano ambapo ligi kuu ya vilabu vya wanawake itaanza kwa kushirikisha klabu 10 huku ligi ya U20 ikishirikisha timu zote zitakazokuwa ligi kuu na sheria itatungwa kama kuna timu yoyote itashindwa kuingiza wachezaji uwanjani itakatwa pointi tatu.

"Kama klabu itashindwa kuingiza timu ya vijana uwanjani itakatwa alama tatu na kanuni hiyo itatungwa rasmi kuanzia msimu ujao pia naamini huu utakuwa ni mwanzo mzuri wa vijana kupata nafasi za kuibua vipaji vyao, na nazitaka timu za wanawake wawe wavumilivu kwani tutaanza na timu 10 kisha tutaendelea kuziongeza kadri siku zinavyokwenda,"amesema Malinzi. Azam media imekuwa ikishirikiana naTFF katika kukuza na kuboresha tasnia ya michezo hususani mpira wa miguu nchini kwa kuingia mikataba kama hii ya urushaji wa matangazo ya moja kwa moja.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wanawake,Amina Kaluma amewashukuru sana kampuni y Azam Media kwa hatua ya kununua haki za matangazo na kuziwezesha timu za wanawake kuanzisha ligi yao itakayokuwa na tija kwa kusaidia kuinua soka la wanawake.

"Nawashukuru sana Azam Media kwa hatua mliyofikia ya kununua haki za matangazo na kuziwezesha timu za vijana na wanawake pia mmekuwa na mchango mkubwa sana kwenye kuinua mpira wa miguu nchini,"amesema Kaluma. Changamoto kubwa ni kutokuwa na waamuzi,makocha,makamisaa wanawake kwahiyo kwa heshima zaidi nawaomba mjitokeze kwenye kozi mbalimbali kwani kama tukiwa mbele zaidi tunaweza kuisimamia ligi yetu wenyewe.

Naye Mkurugenzi wa Azam Media, Rhys Torrington amesema kuwa wanatarajia kupanga ratiba itakayoenda sawa na ligi kuu kwani watakachokiangalia ni kuweza kupanga ratiba ya ligi ya vijana iende sawa na mechi za ligu kuu na hilo anawaomba TFF kuweza kuliangalia hilo.

Mkataba huo utawezesha timu la ligi kuu zilizokuwa zinalalamika kuhusiana na kusafiri na timu za U20 kuanza kwenda nazo kokote kutokana na kulalamika kutakuwa na fedha za kutosha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad