HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 13, 2016

DAWASCO YAJIVUNIA SIKU 100 ZA RAIS MAGUFULI MADARAKANI

Na Joseph Mkonyi -DAWASCO

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), imesema imeweza kutekeleza mipango na maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli, hivyo kuwezesha kupunguza kero na kuboresha huduma ya Majisafi na uboreshwaji wa Majitaka Jijini Dar es Salaam ndani ya siku 100 tangu Rais Dkt Magufuli aingie madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 za utawala  wa  Rais Magufuli, Afisa mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja ametaja mambo yaliyofanikiwa ni pamoja na Kufungua njia za Maji zilizofungwa kutokana uchakavu wa miundo mbinu , Kuzuia mivujo mikubwa na midogo ,kuunganishia wateja wapya huduma ya Maji, ufufuaji wa Mita kuu (Bulk meters), uboreshaji  wa mfumo wa malipo ,uboreshaji wa migao ya Maji pamoja na uboreshaji wa huduma kwa wateja.

“Shirika limeweza kupeleka Maji katika maeneo mengi zaidi ya jiji la Dar es Salaam ambayo hayakuwahi kupata Maji au huduma ilisitishwa kwa sababu ya uchakavu wa miundo mbinu. Katika Kipindi hiki cha Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli, jumla ya maeneo 52 yameweza kupata Maji kwenye wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke mfano maeneo ya Temeke sokota, Kimara B, na Buguruni mnyamani na mengine mengi maana Rais aliagiza tumtue Mama ndoo kichwani”.

“Pia tumeendelea kutekeleza agizo la kufikisha wateja milioni 1 ifikapo juni 2016 hivyo tumeanza kuunganisha wateja wapya na mpaka sasa tumeweza kuunganisha wateja 3500, lakini mradi wa Ruvu chini unatarajia kuisha Februari 2016 mwishoni na kuongeza upatikanaji wa Maji toka lita za ujazo 300milioni mpaka lita 450 milioni hivyo sehemu ambazo hawajafikiwa na huduma ya Maji wataweza kufikiwa”.

“kwa upande wa miradi kwa siku 100 za Mh Raisi Kuna miradi miwili imeshakamilika ambapo ni Mradi wa Kibamba shule uliopo kibamba ambapo unahudumia wananchi takribani  na Mbweni teta uliopo wilaya ya kinondoni ambao nao unahudumia wananchi takribani….

Pia tumeweza kupunguza upotevu wa Maji( Non Revenue Water) kutoka asilimia 57 mwanzoni mwa mwezi September 2015 mpaka asilimia 42 kwa mwezi January 2016 na juhudi zinaendelea kupambana na upotevu wa Maji ili tufikie lengo la chini ya asilimia 20 ifikapo 2018.

 “Tumeweza kuwabaini watumiaji maji 1250 walio nje ya utaratibu (informal Water users) ambao ni watengeneza bustani, watengeneza matofali, hotel na lodge ambazo walikuwa hawalipii huduma ya Maji na kuzisajili rasmi na sasa wana mita kabisa na wanalipia huduma ya Maji kila mwezi hivyo kuongeza Mapato ya Shirika” aliongeza Mhandisi Luhemeja wamekamatwa waliokuwa wanatumia Maji kiholela bila kuunganishiwa na Dawasco”.

“Makusanyo yameongezeka ndani ya siku 100 Shirika limeweza kuongeza mapato yake kutoka bilioni 4 mpaka bilioni 7 kwa mwezi  pia tumeboresha kitengo cha huduma kwa wateja na hivi sasa kinafanya kazi kwa muda wa masaa 24 na hivyo kutoa nafasi kubwa kwa mteja kupata huduma muda wowote anapo pata tatizo au msaada” . Alisema  Mhandisi Cyprian Luhemeja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad