HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 9, 2016

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NA TASWIRA MBALI MBALI ZA VIJANA WAKIVUA SAMAKI KATIKA MFEREJI WA MAJI YOMBO BUZA

Katika pita pita za Mtaa kwa Mtaa, nilibahatika kufika eneo la Yombo Buza Wilayani Temeke jijini Dar. nikiwa eneo la Buza Mwisho nilikutana na kundi la watu likiwa limejikusanya kando kando ya mfereji wa maji unatenganisa kati ya Buza na Mwanagati. nilijisogeza mpaka lilipo kundi hilo ili kufahamu zaidi ni jambo gani lililopo pale, Nilipofika nilikuta kuna kundi kubwa la Watoto wakiwa ndani ya Mfereji huo, nilipouliza kulikoni?? niliambia na baadhi ya watu niliowakuta pale kuwa watoto hao wanavua Samaki ambao walijitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kuyaondoa maji hayo ili mfereji huo ufanyiwe usafi. Nilishangazwa kidogo na hali ile, kwani ilikuwa ni ngeni machoni mwangu, na hapo ndipo nikajiuliza kuwa uvuvi huu ni halali au ni haramu?? lakini ukiachana na hilo, je,usalama wa afya ya vijana hawa uko wapi?? kuna kupona kweli kwa magonjwa ya mlipuko?? bado sikupata majibu na baadae nikaishia zangu kuendelea na majukumu mengine ya ujenzi wa Taifa.
 Hapa zoezi la Uvuvi likiendelea huku baadhi ya watoto hao, wakiwa wamefanikiwa kupata vitoweo vyao.
 Mwanzo nilidhani ni Watoto tu waliokuwa wakijishughulisha na Uvuvi, huo nilipohamia upande wa pili nilikutana na wengine lakini hawa sasa ni vijana wakubwa.
 Hapa napo mambo yamenoga kweli kweli....
Wengine wali kuwa pembeni kusubiria vitoweo hivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad