HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 1, 2015

Balozi Ombeni Sefue azungumzia kuhusu urejeshwaji wa fedha kutoka Uingereza

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.

Amesema kuwa Benki kuu ilifanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma,malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia kwa hiyo tetesi tukazipata, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Kampuni ya Egmwa na siku chache zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa. 


TAARIFA KAMILI SOMA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad