HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 26, 2015

Muhimbili Yapokea Mashine ya kusaidia wagonjwa kupumua

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator  ya kumsaidia mgonjwa kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000  sawa na Shilingi milioni 80.

Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland .

Akikabidhi mashine hiyo  mpya na  kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya miaka miwili.

Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi.


Akielezea  kuhusu mashine hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema  mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo  inaonyesha .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa wagonjwa.
Meneja Mauzo barani Afrika, Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad