HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 30, 2015

HUAWEI YAZINDUA KAMPENI YA “JIEKOTISHE”

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Samson Majwala (katikati) na akionyesha Mkuu wa Bidhaa za Rejareja, Sylvester Manyara wakionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu zilizoingia kwenye kampeni maalum ya Msimu wa Sikukuu ijulikanayo kama “Jiekotishe na Huawei”, wakati wa uzinduzi wake uliofanyika leo Jijini Dar es salaam. Kulia Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Lyidia Wangari.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Lyidia Wangari, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni maalum ya Msimu wa Sikukuu ijulikanayo kama “Jiekotishe na Huawei”, wakati wa uzinduzi wake uliofanyika leo Jijini Dar es salaam. Wengine pichani toka kulia ni Msemaji Mkuu wa Kampuni ya Huawei, Jimmy Jin, Mkuu wa Bidhaa za Rejareja, Sylvester Manyara pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Samson Majwala.
Mabalozi wa kampeni ya “Jiekotishe na Huawei” wakilifanyikisha tukio ya Selfie kwa kutumia simu mpya aina ya Huawei P8 lite.
Huawei Tanzania leo hii imezindua kampeni maalum ya Msimu huu wa Sikukuu ijulikanayo kama “Jiekotishe na Huawei”, uzinduzi huu umefanyika katika ofisi za Huawei zilizoko Golden Jubilee Towers jijini Dar Es Salaam.

Pamoja na uzinduzi wa Kampeni ya “Jiekotishe na Huawei”, Kampuni ya Huawei imezindua pia simu kadhaa mpya. Simu zilizozinduliwa leo ni Huawei P8 Lite ambayo ni Smartphone, pamoja na simu nyingine kwenye familia ya Kishkwambi ambazo ni Kishkwambi Y5C na Kishkwambi Y3C.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi huu, Bwana Samson Majwala, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Huawei alisema “Tunayo furaha kubwa sana leo hii kuzindua kampeni hii ya “Jiekotishe na Huawei”. Lengo hasa la Kampeni hii ni kuwashukuru wateja wetu kwa kipindi chote walichokuwa nasi. Tumepanga kuwapa zawadi mbalimbali kila watakaponunua simu zetu tulizozindua leo hii yaani Huawei P8 Lite ambayo ni Smartphone, pamoja Kishkwambi Y5C na Kishkwambi Y3C.

Akitaja ubora wa simu hizi, Bwana Majwala aliendelea kusema kwamba Smartphone ya Huawei P8 Lite ina uwezo mkubwa wa kutoa picha zilizo bora sana hasa kwa sababu ya kamera yake yenye 13MP, ina uwezo pia wa kutuma picha hizi kwa urahisi kabisa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Alisema pia simu hii ina muundo mzuri sana wa kisasa na inapatika katika bei nafuu kabisa. Wateja watakaonunua simu ya Huawei P8 Lite katika msimu huu wa sikukuu watapewa zawadi ya Selfie stick au Chupa ya Maji.

Bwana Majwala alitaja pia sifa za simu ya Kishkwambi Y5C, alisema hii ina Quad Processor, kifaa hiki husaidia mtumiaji wa simu kupata urahisi wa kutumia na hufanya simu haikwami kwami (kustuck) hasa wakati wa kuchukua picha nyingi kwa muda mfupi. Simu hii inauzwa kwa bei nafuu sana. Wateja watakaonunua simu hii ya Kishkwambi Y5C, katika msimu huu watajipatia Tshirt au Frame ya picha (Photo Frame).

Majwala alimalizia kwa kutaja sifa za simu ya Kishkwambi Y3C kwamba ina flash mbili, hii husaidia kuipa simu uwezo wa kutoa picha nzuri kwa mara moja bila kujaribu mara nyingi kuipata. Simu hii inauzwa kwa bei nafuu sana na wateja watakaonunua simu hii katika msimu huu watajipatia pia Tshirt au Frame ya picha (Photo Frame).

“Tunawakaribisha wateja wetu wote washiriki katika kampeni yetu ya “Jiekotishe na Huawei”, watembelee maduka ya mawakala wetu au wasambazaji wa simu nchini kote kwani huko kutakuwa na promosheni maalum ambapo wateja watakaonunua simu hizi watazawadiwa.” Alimaliza Bwana Majwala.

Waandishi na wageni waalikwa walitambulishwa pia kwa Mabalozi wa kampeni ya “Jiekotishe na Huawei”, hawa ni wasanii waliobuka na nafasi za juu katika shindano la kusaka vipaji linalojulikana kama Bongo Star Search ambalo kwa mwaka huu lilidhaminiwa pia na kampuni ya Huawei. Mabalozi hawa ni Bw. Nassib Fonabo, Bi Frida Amani and Bw. Kelvin Gerrison ambao wote ni wasanii wa jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wengine, Bi Frida Amani aliwaalika wateja wote kujipatia simu hizi kwani zina ubora wa hali ya juu na zinapatikana kwa bei nafuu. “Nikiwa na mabalozi wenzangu tutatembelea madukani ambako tutatoa zawadi mbalimbali kwa wateja, kupata Selfie na washabiki wetu etc” Alimaliza bi Frida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad