HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 2, 2015

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML, WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA.

 Moja kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.

NA K-VIS MEDIA
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.



Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.

” Alisema
“Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua
Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.

Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na gharama ya shilingi 174,392,000.

Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.

Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka mgodi huo.

“Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.

 Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. 









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad