HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 4, 2015

MABADILIKO MAKUBWA YA KISERA KUINUA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI

Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF profesa Fortunata makene akifungua warsha
Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha.
mwasilishaji wa mada Hosana Mpango akizungumza
Mwasilishaji wa mada Hossana Mpango akizungumza na washiriki (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo.
washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasirimali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha
Washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasiriamali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).

Na Mwandishi wetu
SERIKALI imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kisera kuwezesha kukua kwa viwanda vidogo na vya kati nchini.

Kauli hiyo imo katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) kuhusu ukuaji wa sekta hiyo katika muktadha wa upatikanaji wa fedha.

Akiwasilisha utafiti huo mmoja wa watafiti Hossana Mpango alisema kwamba kwenye utafiti wao wamebaini mgongano mkubwa wa kisera na utendaji, unaosababisha kukwama kwa maendeleo ya sekta hiyo.

Alisema ingawa kuna tatizo kubwa la ajira ambalo limefanya watu wengi kukimbilia kujiajiri wenyewe, kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo hasa sera na uwapo wa mlolongo wa taasisi zinazopishana mamlaka na huku wakiwa ndio wanatoa leseni.
 

Alizitaja taasisi hizo zinazopishana mamlaka kama Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mamlaka ya kodi (TRA) halmashauri mbalimbali nakadhalika.

Alisema mabadiliko ya kisera yatawezesha kutengeneza muundo unaojali ukuaji wa sekta hiyo hasa kwa kuangalia kodi zinazolipwa ambazo kwa sasa ni za aina moja bila kuangalia uwekezaji unaohusika.

Sekta hiyo ya wajasirimali wadogo na wa kati yenye watu milioni 3 kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2012 inakabiliwa na tatizo la kutokua kutokana na vikwazo mbalimbali vikiwemo pia kukosekana kwa mafunzo ya ujasirimali na uwezo wa kupata fedha za mtaji.

"Ni dhahiri upatikanaji wa fedha kutoka nje ili kuendeleza mtaji ni tatizo. Lakini tatizo hili linakuwagumu zaidi kutokana na riba kubwa, uchelewefu wa kupata mikopo, rushwa katika utoaji na ukosefu wa nidhamu ya fedha kwa wakopaji” alisema Hossana.

Alisema pamoja na mambo hayo kuna matatizo mengine makubwa yanayokwamisha ukuaji wa sekta hiyo. Matatizo hayo mengine ni gharama kubwa zinaootokana na haja ya kukidhi masharti ya uendeshaji wa viwanda hivyo vidogo na vya kati, tozo zinazojirudia, ukosefu wa soko na elimu ndogo ya wajasirimali.

Alisema mabadiliko ya kisera yatasaidia kuimarisha sheria na kuweka sawa mwelekeo wa sekta hiyo kwa kuzingatia kwamba inahitaji mchango mkubwa wa nje ili kukua.

Alisema mathalani ingawa kuna SACCOS, taasisi hizo zinashindwa kwenda kukopa kutokana na riba kubwa na kuwapo kwa mfumo wa kodi na makato mengine yakiwemo ya tozo usiokuwa na tija.

Alisema suluhu nyingine inayostahili kufanywa ni kwa taasisi za kifedha kufuata tabia njema za kimataifa za utoaji wa mikopo unaozingatia pamoja na mambo mengine ukubwa wa mikopo na malipo kwa kuangalia manufaa ya kiuchumi.

"Ili viwanda hivi vya chini na kati kukua masuala ya kifedha na yasiyo ya kifedha ni lazima yaangaliwe na kushughulikiwa..." alisema.

Matatizo mengine ni pamoja na sekta hiyo kukosa msaada huku taasisi mbalimbali zinazohitaji kushirikiana zikifanya vitu kila mmoja na wake.
Taasisi hizo ni SIDO, TRA, WDF, YDF, BRELA na pia miundombinu inayokera katika maeneo hasa ya vijijini.

Pia ili kukuza sekta hiyo ni vyema serikali ikatengeneza miundombinu inayojkidhi haja ya ukuaji wa sekta hiyo kama maghala, masoko, barabara, maji, umeme kwa lengo la kupunguza gharama za kufanya biashara.

Pia utafiti huo ulishauri kwamba serikali ni lazima kutenga fungu ambalo litatumiwa na taasisi kama SIDO, NEEC na hata maofisa biashara wa wilaya kwa ajili ya mafunzo ya ujasirimali na uendeshaji wa biashara.

Mapema Mkuu wa idara ya utafiti na machapisho wa ESRF Profesa Fortunata Makene, aliwataka washiriki wa warsha hiyo kutoa michango katika kuboresha uelewa ili serikali iweze kutatua kizungumkuti cha ukuaji wa sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad