HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 11, 2015

LOWASSA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KAMPENI MKOANI DODOMA

Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikitua kwenye Uwanja wa Taifa wa Gairo Mkoani Morogoro, ikiwa ni sehemu wa muendelezo wa ziara zake za Kampeni anazoendelea, kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. Mh. Lowassa leo amefanya Mikutano yake hiyo katika Majimbo ya Gairo,Kibakwe, Mpwapwa na Kibaigwa Mkoani Dodoma.
Mh. Lowassa na Mh. Sumaye wakielekea eneo la Mkutano.
Meneja wa Kampeni, John Mrema akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mji wa Gairo.
Wakazi wa Gairo, wakifatilia kwa Makini sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
 
Akiwasalimia wananchi wa Gairo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimsikiliza Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA wa Jimbo la Gairo, Salum Mpanda, wakati akimuelezea changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015. Kulia ni Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.

Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA wa Jimbo la Gairo, Salum Mpanda, akiwahutubia wananchi wake.
"Pipozzzzzzzzz........Pawaaaaa......."
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwaonyesha wananchi wa Jimbo la Gairo, Mkoani Morogoro, Kiberiti chenye picha ya Mgobea Ubunge wa CCM wa Jimbo hilo, na kuwataka wasirubunike kirahisi kwa kupewa kitu cha namna hiyo, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro, wakati wa Mkutano wa Kampeni unaoambatana na kunadi sera za chama chake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Gairo Mkoani Morogoro, leo Septemba 10, 2015.
Vijana wa Mji wa Gairo wakionyesha kadi za kupiga kura wakati Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi baadi ya Wagombea UKAWA wa nafasi ya Udiwani kutoka Kata mbali mbali za Jimbo la Gairo, Mkoani Morogogo leo Septemba 10, 2015.



1 comment:

Post Bottom Ad