HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 1, 2015

BALOZI SEFUE KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA 2015.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Siku ya Wahandisi  Tanzania mwaka 2015 Prof. Bakari Mwinyiwiwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini itakayofanyika Septemba 3 mpaka 4 jijini Dar es salaam.Kulia ni Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania Muhandisi Steven Mlote na kushoto ni Msajili msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Muhandisi Benedict Mukama
Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania Muhandisi Steven Mlote (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi  nchini yatakayofanyika Septemba 3 mpaka 4 mwaka huu.
Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.

Na.Aron Msigwa - MAELEZO,1/9/2015.Dar es salaam.
KATIBU Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Tanzania itakayofanyika  Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe hiyo Prof.Bakari Mwinyiwiwa amesema Kuwa Jumuiya ya Wahandisi nchini Tanzania inafanya maadhimisho hayo kwa mara ya 13 toka kuzinduliwa kwake mwaka 2003 kuenzi mchango wa wahandisi  katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

Amesema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwawezesha waajiri na wahandisi wazalendo na watumiaji wa huduma za kihandisi kutambua uwezo wa wahandisi wazalendo na kampuni zao pia kuwahamasisha wanafunzi wa kitanzania wanaosomea fani hiyo ili waweze  kufanya vizuri katika masomo yao.

Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatajikita katika kuangalia masuala mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa miundombinu,Maendeleo ya viwanda, ukuzaji wa uwezo, na maendeleo ya shughuli za kilimo nchini Tanzani.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Muhandisi Steven Mlote ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo shughuli mbalimbali za kitaaluma zitafanyika ikiwemo majadiliano ya kina kuhusu shughuli za kihandisi nchini na miaka 15 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Amesema wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na utambuzi na utoaji wa Tuzo na zawadi mbalimbali  kwa wahandisi na wahitimu wa Taasisi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao mwaka 2014/2015 pamoja na wahandisi kurejea kiapo cha utii kwa taaluma yao.

Ameongeza kuwa wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho ya kiufundi ya jumuiya za wahandisi wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia St.Joseph na Chuo cha Ardhi (ARU).

Jumuiya nyingine ni ile ya Makandarasi ,Kampuni za Ushauri wa kihandisi,Mashirika na makampuni ya kibiashara na taasisi za utafiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad