HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 14, 2015

TASWIRA MBALI MBALI ZA MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS WA UKAWA JIJINI MBEYA LEO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.







































1 comment:

Post Bottom Ad