Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim
Rungwe akipokea fomu ya kugombea urais kutoka kwa Afisa Mwandamizi Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adam Nyando katika ofisi za NEC leo jijini
Dar es Salaam.
Mgombea
Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe
akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea
Urais kwa tiketi ya CHAUMA nje ya ofisi NEC leo jijini Dar es Salaam.
(Pichana Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda, Globuya Jamii.
MWENYEKITI
wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe amechukua
fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza
baada ya kuchukua fomu hizo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), leo jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema watanzania kama
wanahitaji maendeleo wachague chama hicho na sio kuchagua watu wanaotaka
kutumikia matumbo yao.
Amesema zoezi la kuchukua fomu za urais ziko wazi na kutufanya wagombea
kuwa huru katika zoezi zima kutoka na maandalizi yalifanywa na tume ys
Taifs ys Uchaguzi.
Rungwe
amesema mwaka 2015 aligombea kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi
lakini kura hazikutosha na kufanikiwa kupata wabunge wawili kwa tiketi
kwa chama hicho.
Amesema ana uwezo wa kuwatumikia watanzania na sio kwenda Ikulu kwa
ajili ya kutafuta jinsi ya kujinufaisha na kuwaacha watu walionipa
ridhaa ya kuwaletea maendeleo.
Aidha
amesema nafasi ya urais sio ya mchezo kutoka na na kuwa majukumu
makubwa ya kuwatumikia watu katika kuwapa maendeleo yatayotokana nafasi
hiyo.
“Nina
imani watanzania wataichaugua CHAUMA katika kuperusha bendera katika
kuweza kupata maendeleo kama kauli mbiu ya chama kutaka ukombozi”
anasema Rungwe.
Vyama vilivyochukua fomu ya urais vimefikia vinnea mbavyo ni, Chama cha
Tanzania Labour Party (TLP), UPDP, Chama cha Democratic Party (DP),
pamoja na Chauma.
Mgombea
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli anatarajia
kuchukua fomu kesho katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), jijini Dar es Salaam.
mwisho
No comments:
Post a Comment