HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 4, 2015

MKUTANO MKUU WA CHADEMA WAMPITISHA BILA KUPINGWA MH. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS WA TANZANIA NA DKT. JUMA HAJI DUNI MGOMBEA MWENZA

Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa (kati) akiwa ameshikana mikono Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar alieteuliwa na Chama ya Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Dkt. Juma Haji Duni, mara baada ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa nne kulia) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (mwenye suti nyeusi) pamoja na wanachama wapya wa Chama hicho, wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake ya shukrani wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CHADEMA na UKAWA, Dkt. Juma Haji Duni akitoa hotuba yake ya shukrani wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
 Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar alieteuliwa na Chama ya Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza.
 Picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais wa CHADEMA, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad