HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 24, 2015

demo-image

MATUKIO KATIKA PICHA: LOWASSA, BABU DUNI WAFANYA ZIARA MAENEO YA GONGO LA MBOTO NA MBAGALA JIJINI DAR LEO

MMGL1447
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.
MMGL1457
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo.
MMGL1557
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo.
MMGL1612
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.
EDWI4576
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi.
MMGL1677
Mh. Lowassa akishuka kwenye daladala.
MMGL1765
MMGL1769
Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo

MMGL1802
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.
MMGL1814
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.
MMGL1844
MMGL1862
MMGL1864

2 comments:

  1. blank

    ..nampenda sana lowasa yupo smart sana huyu baba..hataki fujo, vurugu, wala matusi. ccm walimwacha akawa kimya...mungu atawaongoza UKAWA penye nia ipo njia...amani itawale..

    ReplyDelete
  2. SAM_2142

    Baba unakubalika, safari tu ya kushtukiza nyomi kuuubwa.... U are the coming president of Tanzania

    ReplyDelete

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *