HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 31, 2015

Makundi 10 yapenya nusu fainali Dansi 100%

Wasanii wa Kundi la The W.D kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oystebay Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Baadhi mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakifuatilia mchuano wa robo fainalai ya shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV nakudhaminiwa na Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaunda kundi la Timu Makorokoro wa wilaya ya Temeke jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.

Vijana wanaaunda kundi la timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo iliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robofainali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Da res Salaam ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kundi la wasichana pekee la Cute Babies kutoka Keko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao wa kudansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika katika viwanja Don bosco Oysterbay jijini ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni, Shindano hilo liliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Makundi kumi kati ya makundi 15 yaliyoshiriki katika kinyang’anyiro cha kuingia katika nusu fainali ya mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa  na kituo cha televisheni cha East  Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo mwishoni mwa wiki tulishuhudia hatua ya robo fainali kufanyika katika  uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.

Makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali ni Wazawa Crew,Majokeri,Quality boys,The best,The best boys kaka zao,Team Makorokocho,The winners, The W.D, Cute babies na Team ya shamba.

Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo walipata  makundi 10 hayo ambayo yameingia moja kwa moja katika ngazi ya nusu fainali.

“Huu ni mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki”Alisema Shame.

Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa  moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.

Aliwataka vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad