HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 2, 2015

AZAM FC YATWAA UBINGWA WA CECAFA KAGAME CUP 2015 KWA KUICHAPA GOR MAHIA YA KENYA BAO 2-0


 Kiungo hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiondika na mpira huku Mabeki wa Timu ya Gor Mahia wakiangalia namna ya kumdhibiti, katika mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
 Wachezaji John Bocco (Azam) na Collins Okoth (Gor Mahia) wakiwa chini huku wakiendelea kuonyesha umahiri wao wa kuucheza mpira hapa wakiwa wamelala, wakati wa mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
 Beki wa Timu ya Azam FC, Agrey Morris (13) akiondoa hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni mwao na Mshambuliaji wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya, Godfrey Walusimbi.
Wachezaji wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam wakisherehekea ubingwa wao wa Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, mara baada ya kuitungua timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya Bao 2-0, katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,Mhe. Eugene Segore Kayihura (wa pili kulia) akikabidhi kitita cha Dola za Kimarekani eflu 30 kwa Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" ikiwa ni zawadi ya ushindi wa kwanza iliyotolewa na Mdhamini Mkuu wa Mashindao hayo ambaye ni Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame. Wengine pichani toka kushoto ni Rais wa Cecafa, Leodger Tenga, Mgeni Rasmi kwenye Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick, Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Mgeni Rasmi kwenye Mchezo fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup 2015, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia) akishirikiana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga wakimkabidhi Kombe la Ubingwa huo, Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" baada ya kuichapa bao 2-0 timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.
 Wanakosa goli pale hawa Gor Mahia...........
 Kiungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akionyesha uwezo wake mbele ya Mshambuliaji Machachari wa timu ya Azam FC, Kipre Tchetche, wakati wa mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
 Sasa ni Kipre Tchetche na Karim Nizigiyimana.
 iungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akiachua shuti kuelekea lakongoni mwa timu ya Azam FC.
 Kiungo hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiruka juu kuwania mpira dhidi ya Mshambuliaji wa Gor Mahia, Michael Olunga.
 Washabiki wa Azam FC wakiishangilia timu yao.
 Erasto Nyoni wa Azam FC akionyeshana uwezo na Kagere Medie wa Gor Mahia wakati wa mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
 Mpiga picha akiendelea kuchukua taswira mbali mbali za mtanange huo.

 Washabiki wa Timu ya Gor Mahia wakionekana kuhuzunika baada ya timu yao kushindwa kufua dafu mbele ya wanalambalamba wa Azam FC.
 Azam ni shangwe tupu.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad