HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 6, 2015

Jerry Slaa atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ukonga

Diwani wa  kata ya  Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa akihutubia wananchi katika uwanja wa shule ya msingi kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
Mmoja wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya wenzake  kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala  ambazo alikuwa amewaahidi wakati wa mkutano wa  Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
Baadhi ya madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga
Meya wa Ilala, Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pamoja nae ni Mbunge wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa NEC wa CCM,Mh. Adam Kimbisa.
 Watoto wakitoa burudani wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya Jerry Slaa
Baadhi ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.

Diwani wa kata ya Gongo la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza katika kipindi cha miaka 5 tangia achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.

Slaa alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi kuvisaidia,Genereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi kwenye maeneo yasio na umeme,vifaa ya michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi wa barabara  zitakazojengwa kwa madiwani wa kata za jimbo la Ukonga.


Slaa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga  jana ambapo pia alitangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


 Baadhi ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika shule mbalimbali yameboreshwa,afya-ambapo vituo  vipya vimejengwa na vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji  na ujezi wa barabara kwenye kata  ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.


“Kutokana na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo”Alisema.

Alisema  wakazi za jimbo la Ukonga  wanahitaji  Mbunge ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. “Bado tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii  kama vile   shule, hospitali ,maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya akina mama na vijana kwa kuwa naelewa  matatizo ya jimbo hili na baadhi yake nilishaanza kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitaendeleza safari ya kuleta maendeleo.”

Mkutano huo wa Meya Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.

1 comment:

Post Bottom Ad