HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2015

MWENDESHA MASHTAKA MKUU MISRI KWA MRIPUKO WA BOMU

 

 Gari la mwendesha mashtaka wa Misri likiwa limeharibiwa vibaya na mripuko.

Na Mwandishi wetu. 

Mwendesha mashtaka mkuu wa Misri Hisham Barakati amefariki baada ya mripuko mkubwa wa bomu kuushambulia msafara wake mjini Cairo mapema Jumatatu wakati akielekea kazini.

Shambulizi hilo limefuatia wito wa wapiganaji wa jihadi kuwashambulia maafisa wa mahakama kuwaadhibu kutokana na ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa makundi ya Kiislamu.

Waziri wa sheria wa Misri Ahmed al-Zind ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa Barakati amefariki dunia. Wazitri wa uwekezaji Ashraf Salman naye amethibitisha kifo cha mwanasheria huyo mkuu wa serikali ya Misri, ambaye ndiyo afisa wa ngazi ya juu wa kwanza kuuawa tangu wapiganaji wa jihadi walipoanzisha uasi kufuatia hatua ya jeshi kumuondoa madarakani rais Muhammad Mursi mwaka 2013.

Pigo kwa rais Al-Sisi
Mauaji ya Barakati yatakuwa pigo kwa rais Abdel-Fattah Al-Sisi, mkuu wa zamani wa jeshi aliempindua Mursi na kushinda uchaguzi kwa ahadi ya kuwamaliza wapiganaji wa Kiislamu. Mripuko huo wa bomu uliharibu magari kadhaa na kuvunja vioo vya madirisha ya maduka katika wilaya ya Heliopolis, na ripoti zinasema magari matano yaliharibiwa kabisaa katika mripuko huo.

Katika hospitali alikokimbizwa Barakati kwa ajili ya matibabu, mlinzi wake aliejeruhiwa vibaya aliwaleza waendehsa mashtaka jinsi mripuko ulipoushambulia msafara wa Barakati wakati akielekea kazini, na kusema ilikuwa kama vile kumetokea tetemeko la ardhi.

Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio hilo wamesema moja ya magari yaliyoungua kabisaa lilikuwa la Barakat. Mkuu wa kitengo cha mabomu Jenerali Mohammed Gamal ameliambia shirika la AFP kwamba mripuko huo ulikuwa ama wa bomu la kutegwa kwenye gari au bomu lililofichwa chini ya gari.

Magari mengine yaliyoharibiwa katika mripuko dhidi ya msafara wa Barakat.

Maafisa wa mahakama walengwa
Barakati amefariki kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa vioungo kulikosabishwa na majeraha mabaya, amesema daktari aliekuwa anamtibu. Mripuko huo umekuja baada ya kundi mshirika wa Dola la Kiislamu - Wapinzani wa Giza - kutoa wito wa mashambulizi dhidi ya maafisa wa mahakama kufuatia kunyongwa kwa watu sita wanaodaiwa kuwa wanamgambo.

Wanamgambo wenye silaha katika mkoa wa Sinai ambako wapiganaji wa jihadi wana makao yao, waliwapiga risasi na kuwauwa majaji wawili pamoja na mwendesha mashtaka mwezi Mei. Kundi hilo lilitoa mkanda wa video jana Jumapili ukidai kuonyesha shambulizi hilo katika mji wa El-Arishi mkoani Sinai.


Barakati amewashtaki maelfu ya wafuasi wa makundi ya Kiislamu tangu jeshi lilipompindua Mursi mwaka 2013, ambapo mamia wamehukumiwa adhabu ya kifo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad