HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 29, 2015

PPF YANYAKUA TUZO YA UBORA WA HUDUMA YA ISO KIMATAIFA

MFUKO wa Pensheni wa PPF, umepewa cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa wananchi (ISO) baada ya kukidhi mashariti na vigezo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio alitoa taarifa hiyo leo Ijumaa  na kusema kuwa walipewa tangu Machi 28, mwaka huu.


Alisema wamepewa cheti chenye namba 9001:2008 na kuanzia mwezi Mei, mwaka huu huduma za PPF zinaza kutambulika kimataifa.

“ISO walikuja nchini wakatukagua wakalidhika na viwango vya huduma zetu tunazotoa na wakatupatia cheti cha ubora,” alisema Erio.


Alisema kwa sasa wanachma wa PPF wategemee kupata huduma bora pamoja na uwajibikaji ulio bora.

Alisema kila baada ya miezi sita ISO watakuwa wanatembelea PPF na kukagua kama huduma bora bado zinatolewa, na kila baada ya miaka mitatu PPF watatakiwa ku-renew maombi ya ISO.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa wananchi (ISO) walichokipata baada ya kukidhi mashariti na vigezo
Mameneja wa PPF, na waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio juu ya tuzo hiyo
Wakurugenzi na Mameneja wa PPF
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati), Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Julius Mganga (kushoto) na Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga (risk management), Ufoo Swai wakionyesha cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa wananchi (ISO) wakati wa mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Mei 29,2015.
Erio akizungumzia mafanikio ambayo Mfuko umepata hadi kutunukiwa tuzo hiyo
Tuzo ya ubora ISO katika utoaji huduma kimataifa, ambayo PPF imepata

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad