HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 27, 2015

LORI LAPIGA MWELEKA LIKIJARIBU KUKWEPA GARI NYINGINE KIJIJI CHA KITUMBI

 Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 112 BAL lililokuwa na tela lenye namba za T 108 AVT likiwa halitamaniki baada ya kupata ajali alfajiri ya leo kwenye kijiji cha Kitumbi, Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. Kwa mujibu wa utingo wa lori hilo, aliefahamika kwa jina la Makeke Moses, amesema kuwa kutokea kwa ajali hiyo kulisababishwa na Lori lingine (halipo pichani) lililokuwa limeharibika na kusimama katikati ya barabara bila ya kuwa na ishara yeyote ya tahadhali, hali iliyompelea dereva wake kutumia maarifa yake ya kiudereza ili kulikwepa lori hilo, lakini maarifa hayo hayakuzaa matunda na kujikuta wakitoka kando ya barabara mpaka kufikia hapo. hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo.
 Kichwa cha lori hilo kikiwa pembeni baada ya kutolewa.
 Zoezi la ufaulishaji mizigo likaanza na hapo barabara ikafungwa kwa muda ila kufanikisha zoezi hilo.
 Baadhi ya Matingo wa malori mengine wakimjulia hali Utingo mwenzao alienusurika ajalini.
 Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa kwenye lori hilo.
 Baadhi ya wasafiri wakiwa wamesimama nje ya vyombo vyao kuangalia zoezi hilo.
 Foleni ilikuwa kubwa sana kwa pande zote za barabara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad