HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 22, 2015

Kampuni ya maji ya Kisima AQUA COOL LTD yatoa msaada wa nguo za kujikinga na mvua kwa wafanyabiashara wadogo wadogo jijini dar

Na Niccomeditz

KUTOKANA na mvua kubwa zilizonyesha karibu maeneo yote ya nchi na kuleta maafa hususan katika jijin la Dar es Salaam Kampuni ya Aqua Cool Ltd Watengenezaji wa maji safi ya Kisima Pure Drinking Water imetoa msaada wa mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) kwa wakazi wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Msaada huo ulitolewa na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa makundi mbalimbali kama watembea kwa miguu, mama lishe , waendesha bodaboda na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini wakati wa kutoa msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ali Dhanji alisema kampuni imefanya hivyo kama sehemu ya shukrani kwa jamii, kuwajali wateja wao pia kwa wananchi wa kawaida walioathirika na kutatizwa na kadhia ya mvua inayoendelea kunyesha .

Wafanyakazi wa kampuni ya maji ya Kisima AQUA COOL LTD wakitembea wakiwa wamevaa mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) Kushoto ni Meneja Masoko Bw. Sachin Smart , katikati ni Mkurugenzi Mkuu Bw.Ali Dhanji na kulia ni Meneja wa uzalishaji Bw. Mohamed Saleh .
Aliongeza kusema wamefanya hivyo ili kuwarejeshea urahisi wa kufanya shughuli zao ambazo kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua na kuwakwamisha kuendelea na shughuli za kujipatia kipato kwa muda hivyo kuyumba kiuchumi.

"Tusingependa kuona athari za mafuriko kushusha uchumi na shughuli zenu kama ilivyokuwa mwaka jana , ndio maana tunaishukuru manispaa ya Temeke kwa kuliona hilo mapema na kuboresha miundombinu ya barabara ya changombe ili watu waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida," alisema Ali.

Mfanyabiasha mmoja akiendelea kufanya biashara yake bila wasiwasi huku akiwa amevalia nguo ya kuzuia mvua wakati mvua ikiendelea kunyesha katika maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Aidha aliongeza kuwa wamejizatiti wataendelea kusambaza takribani mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) 6000 katika maeneo mengine ya jiji ndani ya wiki moja kwa kuzingatia kuwa faida ya shilingi 20,000 anayoipata mtu kwa siku moja ni kubwa sana ukilinganisha na gharama ya mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) moja ambayo ni shilingi 2000.

Aidha alisema msaada huo ni sehemu ya kutekeleza mradi wao wa KISIMA CARES 2015 wa kurushirikisha wateja wake faida wanayoipata kutoka kwenye jamii pamoja na kutoa misaada mingine kama maji ya kunywa na malazi kwa yatima na walemavu katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Kampuni ya Aqua Cool Ltd watengenezaji maji safi ya Kisima inatarajia pia kutoa misaada kwa wananchi hususani vijana na ili waweze kuongeza kipato na kuinua hali zao kiuchumi . Kwa maelezo tembea tovuti ya kampuni : www.kisimawater.com au Facebook Page "Kisima Pure Drinking Water.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad