HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 25, 2015

WATANZANIA 26 WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAREJEA NYUMBANI, 20 WENGINE KUHAKIKIWA NA KUREJESHWA

Kundi la Watanzania 25 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad