HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 19, 2015

Waingereza wajitosa kusaidia vijana wasio na ajira

Na Ripota Maalum.

Serikali ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasaidia vijana wa Tanzania katika kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira kwa kuwapa maarifa na mikakati ya kujiajiri na kujinadi kwa waajiri .

Vikwazo vinavyowakabili vijana katika soko la ajira ni pamoja na kutokuwa na maarifa ya kupata kazi na tabia ambazo zitawawezesha kuwa karibu na wafanyakazi wenzao,kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo kuweka heshima na mwisho kuwa wawakilishi bora wa taasisi wanayotumikia .

Kwa kutambua changamoto hizo Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka taasisi ya Restless Development Organization (ICS)kuwafundisha vijana mikakati ya kujinasua na matatizo hayo .

Wakizungumza katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) walimu hao wa kujitolea wamesema wanawafundisha vijana namna ya kuandika wasifu wao wenye maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu, ujuzi na kujiajiri wenyewe .
Kiongozi wa walimu (ICS) Gemma Bunn aliliambia gazeti hili kwamba sababu ya kuwapo hapa nchini ni kwa kutambua kuwa Tanzania ina vijana zaidi ya asilimia 50 ambao hawawezi kupata ajira na wengi hukwama kutokana na vigezo kama hivyo .

‘’ Tunatoa mafunzo kuhusu maarifa ya kupata ajira ikiwamo namna ya kuandika maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu , ujuzi , kujiajiri wenyewe na namna ya kujiweka wakati wa kufanya usaili pamoja na mbinu za kuanzisha biashara na kujengeneza bajeti ‘’ alisema Bunn.

Mwalimu Wendy Morrissey anasema wasifu (CV) ni nyaraka muhimu kwa wanafunzi hivyo ni wajibu kujifunza kuandika . Ni nyaraka itakayowasaidia kupata ajira na kutaja mambo ya kuyazingatia na kuyaweka kuwa ni pamoja na ujuzi na maarifa kwa nafasi ya kazi unayoombea .
‘’ CV haitskiwi iwe ndefu zaidi ya ukurasa mmoja kwasababu mwajiri anachukua muda wa sekunde nane kuiangalia . Kwa hivyo unatakiwa kumvutia mwajiri kwa kutumia muda mfupi anapoisoma ‘’
Wakati ukiandika nyaraka hiyo unatakiwa ueleze kwa weledi na usiandike kwa kutumia maneno ya mtaani .

Mambo mengine ambayo hayatakiwi kuonekana ni sarufi ambazo sio sahihi kwenye maelezo hayo anawashauri kupitia kwanza maelezo yote pamoja na sarufi kabla ya kuikabidhi kwa mwajiri .
Jambo lingine la  kuepuka ni kuandika maeezo kwa matakwa yao ambayo hayaendani na kazi unayoomba .

Jonathan Aquilina mmoja wa walimu hao wa kujitolea anayefundisha namna ya kujiajiri mwenyewe anasema njia rahisi ya kukabiliana na changamoto ya mikopo ni kujiunga katika vikundi .
‘’ Inaweza kuwa ni kikundi cha marafiki au familia na pale kinapokuwa kikundi kikubwa hatari inakuwa ndogo . Hiyo ndio njia rahisi ya kupata mikopo ‘’ anasema Aquilina .

‘’ Njia rahisi ya kujiajiri mwenyewe ni kulifahamu soko lako . Lazima umjue unaye muuzia bidhaa zako na ufahamu wanahitaji nini . Kama hautafahamu hautaweza kuuza chechote . Unatakiwa kufanya utafiti wa soko na kufahamu washindani ni wakina nani na bei wanazouza bidhaa ni zipi ?
Anasema siku zote tathmini biashara yako . Uimara na udhaifu na pia ufahamu kinachoendelea kwenye soko .

Philip Luke , mratibu wa mafunzo katika chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management ( KITM) wanakofundishwa vijana hao na mwezeshaji wa mafunzo Dani Kishimbo wanasema mafunzo yamekuwa na umuhimu mkubwa kwasababu wafanyakazi pamoja na wanafunzi wamepata maarifa mapya namna ya kuandika wasifu na kuanzisha biashara zao .

‘’ Tumepata maarifa mapya ya namna ya kuanzisha biashara zetu wenyewe na pia namna ya kujiweka na kujibu maswali wakati wa usaili . Tunafahamu namna ya kujipanga wakati wa kujibu maswali inavyotakiwa ‘’ anasema Luke .

Dani Kishimbo m mratibu wa mafunzo anasema yamekuwa na umuhimu mkubwa na maarifa waliyoyapata wanafunzi watayatumia kuomba mazoezi kwa vitendo au ajira .

Taasisi ya Restless Development  mtazamo wao ni kusaidia vijana kuchukua jukumu la kuwa viongozi kwa kutatua changamoto zinazozikabili chi zao na dunia kwa ujumla .

Taasisi hiyo inatekeeza mtazamo huo kwa kuwajengea uwezo vijana kimaarifa , kimsukumo na raslimali kuchukua nafasi za kazi ambazo zinachangia sio tu kupata kipato cha familia bali pia uchumi wa jamii pamoja nan chi zao.

Mafunzo hayo yamekuja huku kukiwa na ripoti ya Baraza la vyuo vikuu vya Afrika ya mashariki ikisema karibu nusu ya wahitimu wanaozalishwa na vyuo vya nchi hizo hawana uzoefu katika soko la ajira .

Ripoti hiyo inasema wakati maelfu ya vijana wanamaliza kila mwaka , sifa wanazokuwa nazo haziwezi kuwasaidia kuwapa kazi nawaajiri wanawaacha na kuchukua wenye ujuzi jambo ambalo linaleta changamoto ya ukosefu wa ajira katika ukanda huu .

Kwa mujibu wa katibu wa baraza hilo , profesa Mayunga Nkunya , waajiri wanasema wahitimu wengi wa vyuo wanakosa kujiamini , hawawezi kujieleza vizuri na hawana ujuzi wa kitaalam unaotakiwa karika kazi wanazozitafuta .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad