HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 27, 2015

NHIF yazindua awamu ya pili ya Kampeni ya uhamasishaji Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatina muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.

Ulega ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani kilwa.

Ulega amesema Serikali kupitia mfuko wa uchangiaji wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Bima ya Afya, Rehani Athumani alimweleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa kampeni hiyo iliyozinduliwa leo itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

Rehani alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.

Naye mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga aliwaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Afya wa Jamii katika mikoa hiyo. 

Aliomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.

Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa, wakati uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akielezea namna kampeni hiyo inavyofanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15, katika uzinduzi uliofanyika leo katika Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mashuka 150 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani(kulia) kwa ajili ya Zahanati za Wilaya ya Kilwa.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani (katikati). kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega.
 Afisa Matekelezo na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ofisi ya Mkoa wa Lindi, Paul Marenga akiongoza shunguli nzima ya uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
 Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega (kulia) akimtambulisha Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Lindi, Dkt. Peter Nsanya kwa wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa na kuwatakama kama wanamatatizo yeyote ya kimatibabu waweze kumuona.
 Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega akiwaeleza jambo baadhi ya Wazee wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa, ambao hawakuwa na uwezo wa kujilipia gharama ya kujiunga na huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kuweza kuwalipia gharama hizo.Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani, anaefuata ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond.

 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa wakifatilia kwa makini uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
 Sehemu ya kina Mama wakazi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa wakishindana kukuna nazi ili kujipatia fursa ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Fadhil Mtitu akimpima uzito na urefu mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa wakipima afya zao katika uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad