HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

IMETOSHA WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM CHA BUHANGIJA MKOANI SHINYANGA





Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

 Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.  “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.

 Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa” alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10. 
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha wakiwa kwenye Kituo hicho.

Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.

Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284 wana ulemavu wa ngozi. 

Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.



 Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika kituo hicho
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha
  Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo
  Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga
 Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.


Wajumbe wa Imetosha


Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands!
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga


Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho
Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali
Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad