HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 3, 2015

WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU JIJINI ARUSHA KUJENGEWA HOSTEL

Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.

Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto hao kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Sawale alisema kuwa iwapo watoto hao watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .

"Watoto hawa tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya" Alisema Sawale

Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa  Panju  alijitolea kuwasaidia watoto hao kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 ili waweze kupata mahitaji muhimu  ,Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa .
 Kikundi cha ngoma cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Baadhi ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Arusha waliokusanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto hao kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad