HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 5, 2015

WAFANYABIASHARA WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAITAKA SERIKALI KUPUNGUZA KODI

Na Tinah Reuben, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon Chonde amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja limepitishwa kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na wafanyabiashara hao.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo wa kodi uliopo umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili waendelee kuwa tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyabishara wadogo.
Chonde amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni ameitaka Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili kumsaidia mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
Naye Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado ni machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la zima moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
Pia amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam (JWT), Philimon Chonde akizungumza katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu akisisistiza jambo katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akifanya majumuisho katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wafanyabiashara akiombea mkutano kabla haujaanza.
 Mbunge wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akisalimia na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
 Waheshimiwa wabunge wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mkutano, kutoka kulia ni Mhe. Abbas Mtemvu, Mhe. John Mnyika na Mhe, Mussa Azan Zungu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
 Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika mkutano huo.

1 comment:

  1. Masahihisho:

    Anayetajwa katika picha kwa jina la Philemon Chonde, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam si yeye.

    Aliyeko kwenye picha anaitwa Mashaka Kingoni Mwaisaka.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad