HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 28, 2015

BONDIA MOHAMED MATUMLA AMKALISHA MCHINI USIKU HUU

Mwamuzi wa Mpambano wa Masumbwi uliowakutanisha mabondia Mohamed Matumla (Tanzania) na Wang Xin Hua (China) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu,akiwa amemnyanyua mkono Bondia Mohamed Matumla baada ya kumchapa kwa Point bondia mwenzake kutoka nchini China katika mpambano wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.
Wanahabari wakichukua taswira mbali mbali za mpambano huo.
Bondia Mohamed Matumla akiangalia namna ya kumrushia konde mpinzani wake Wang Xin Hua (China) wakati wa mpambano wao wa raundi 10 wa kuwania nafasi ya kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao unakaochezwa mapeka mwezi Mei mwaka huu, huko nchini Marekani.Katika Mpambano huu, Bondia Mohamed Matumla alishinda kwa point.
Matumla akimchezesha Wang Xin Hua.
Wang Xin Hua akimrushia konde zito Mohamed Matumla bila mafanikio.
wakiendelea na mpambano huku kila mmoja akimvizia mwenzake.
Wang Xin Hua akirusha konde kwa Mohamed Matumla ambaye leo alikuwa makini sana kuhakikisha hampi point hata moja mpinzani wake.
Chukua hiyoooo....
Wang Xin Hua anajibu mashambulizi kwa kasi ile ile ya Matumla.
Matumla akionyesha uhodari wake kurusha makonde kwa mpinzani wake.
Matumla tenaaa.....
Matumla anatakata hapa,anampa ambakati moja maridadi kabisa.
 Mbali na mpambano kati ya Matumla na Mchini, kulikuwepo na Mpambano uliowakutanisha mabondia Mada Maugo na Japhet Kaseba ambao ulikuwa ni wa raundi kumi wa uzito wa kati,Katima mpambano huo, Bondoa Mada Maugo aliweza kumgaragara Japhet Kaseba kwa Tekniko Nokauti (Technical Knockout) katika raundi ya nane (8) ya mchezo wao huo.
 Kwa konde hili lazima mtu akaeee......












 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad