HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 19, 2015

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe akizungumza na wazalishaji na watumiaji wa takwimu leo jijini Dar es salaam. Warsha hiyo imewakutanisha wadau hao kutoka maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu nchini.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho Said akifungua warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka Wizara, Idara za Serikali, Wakala, Taasisi za Elimu na Utafiti, Vyuo Vikuu pamoja na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya Elimu ya Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo leo jijini Dar es salaam.

Na Aron Msigwa,Dar es salaam. 

 SERIKALI imetoa wito kwa watafiti na wataalam kutoka vyuo vikuu, taasisi za elimu na mashirika binafsi kushiriki kikamilifu kuhamasisha jamii kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kuwezesha upangaji wa mipango endelevu ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya maeneo husika.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati akifungua warsha ya siku mbili ya wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Vyuo vya Elimu ya Juu, Taasisi za kiraia,Taasisi za Utafiti na Wadau wa mbalimbali wa maendeleo, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Hajjat Amina Mrisho Said amesema kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya takwimu sahihi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Amesema wadau hao pamoja na mambo mengine wanalo jukumu la kuielimisha jamii kuelewa mchango wa takwimu katika kufanikisha masuala mbalimbali ya taifa pamoja na uandaaji wa sera za maendeleo.

Bi. Hajjat amesema Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekuwa ikifanya mabadiliko makubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa takwimu zinazokusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji nchini.

“Tanzania sasa inafanya maboresho na mabadiliko makubwa ya takwimu zake sasa tunazo takwimu mbalimbali na mkakati wa kuzisambaza takwimu hizo kwa watumiaji ili waweze kuzifanyia kazi unaendelea” Amesema .

Akizungumza kuhusu umuhimu warsha hiyo amesema inalenga kuwaweka pamoja wazalishaji na watumiaji wa takwimu kutoka katika maeneo mbalimbali ili waweze kujadili changamoto mbalimbali, kubadilishana uzoefu na kupeana mrejesho wa matumizi ya takwimu zilizopo hapa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Ofisi Bw. Michael Madembwe akizungumzia umuhimu wa warsha hiyo kwa washiriki hao amesema kuwa imewakutanisha wadau hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na kupima mafanikio ya shughuli za kitakwimu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Ameongeza kuwa warsha hiyo ya siku 2 inalenga kuwawezesha wadau hao kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usambazaji na ukusanyaji wa takwimu katika maeneo mbalimbali nchini, kubadilishana uzoefu na kuangalia mahitaji yanayojitokeza pande kwa wazalishaji na watumiaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad