HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 26, 2015

NHIF KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOA YA PEMBEZI WA NCHI

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitabibu na Kitaalam wa NHIF,Dkt. Aifena Mramba (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumzia juu ya huduma ya madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni.Kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF,Angela Mziray.

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatarajia kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni kwa ajili ya kutoa huduma za kitaalam kwa wakazi wa maeneo hayo.

Kupeleka kwa madaktari hao kunatokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za uchache wa madaktari hao,umbali wa hospitali kubwa zenye huduma hiyo au changamoto za Kijiografia zinazozuia kufika kirahisi pamoja na za kimiundombinu.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitabibu na Kitaalam wa NHIF,Dkt. Aifena Mramba amesema mikoa ambayo ilipata huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika awamu ya kwanza ni mikoa ya Lindi na Kigoma,ambapo awamu ya pili ilikuwa ni mikoa ya Rukwa,Katavi na Pwani. 

Awamu ya tatu ya mpango huo ambayo ilianza mwisho mwa mwaka jana ilihusisha mikoa ya Mara,Tabora,Manyara na Mtwara,ambapo waliopata huduma hiyo ni 5,829 kati ya hao 153 walifanyiwa upasuaji.

Dkt. Aifena amesema kupeleka huduma ya madaktari bingwa ni kutokana na mafanikio yaliyotokana na NHIF kubaini kuwa kuwa Watanzania wengi wanahitaji huduma za madaktari bingwa na madhumuni ya mpango huo ni kushiriki katika kufanikisha lengo la serikali la utoaji wa  huduma bora za afya kwa watu wote na kuleta wa  unafuu kwa wananchi wa pembezoni au mikoa iliyo mbali na huduma za hizo.
 
NHIF inagharamia uwepo wa madaktari hao,vifaa tiba na dawa zinazotumika katika zoezi hilo na mwitikio  wa wananchi ni mkubwa ikilinganishwa na madaktari bingwa  pamoja  na changamoto za vifaa tiba vya kisasa katika baadhi ya hospitali,uhaba wa vitendanishi vya kupimia,miundombinu na uhaba wafanyakazi wenye uzoefu ili kusaidiana na madaktari bingwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad