HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 30, 2015

TTB YAENDELEA NA ZIARA YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA NCHINI MAREKANI

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiongea katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akiwa pamoja na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki ziara maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiwasilisha mada inayohusu vivutio vya utalii nchini katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ndege ya Emirates Ndg. Akbar Hussein akiongea juu ya namna gani unaweza kufika Tanzania kwa kutumia usafiri wa Emirates.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ndege ya Ethiopian Airlines akiongea juu ya namna gani unaweza kufika Tanzania kwa kutumia usafiri wa Ethiopina Airline.
Baadhi ya washiriki wa hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani iliyofanyika katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiongea na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani iliyofanyika katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Mwakilishi wa Ethiopian Airline (kati) akiongea katika hafla hiyo.Wengine pichani ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi.

1 comment:

  1. Hii ni habari njema.

    Napenda kuongezea kuwa makampuni ya Marekani yanayopeleka watalii Tanzania yanafanya kazi kubwa ya kuvitangaza vivutio vya Tanzania. Ninafuatlia kwa makini shughuli za baadhi ya makampuni hayo, na mawili kati yao nimewahi kuyasaidia baada ya kuniomba.

    Jambo jingine ni kuwa watu waliokwisha safiria Tanzania ni watangazaji wakuu wa vivutio vya nchi yetu. Watu hao ni pamoja na watalii, wanafunzi, na wanaofanya shughuli za kujitolea. Utangazaji huu, unaoitwa "word of mouth" kwa ki-Ingereza, ni muhimu sana katika biashara yoyote.

    Jambo la tatu ni kuwa tungekuwa na ndege zetu za kuwasafirisha watalii tungefaidika sana. Ukisafiri na "Ethiopian Airlines," kwa mfano, unaona humo ndani wanavyoitangaza nchi yao na vivutio vyake. Inasikitisha jinsi Tanzania tunavyojikosesha fursa ya namna hii, na badala yake wanafaidi wenzetu.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad