HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 10, 2015

MH. SUGU APATA AJALI MBAYA MLIMA KITONGA MCHANA WA LEO

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa mchana wa leo.kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa Mh. Mbilinyi alikuwa safarini akitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar akiwa na jamaa zake Wanne katika gari hilo lenye namba za usajili T 148 BQE. katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.
Gari hiyo inavyoonekana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad