HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 26, 2015

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO MKUU WA MAKAMANDA WA POLISI KWA MILIONI 75

Benki ya NMB leo imekabidhi hundi ya shilingi Milioni 75 kama udhamini wa mkutano wa mwaka wa maafisa wa Polisi nchini unaendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Kimataifa wa St Gasper.

Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu, umezinduliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Mathias Chikawe.

Akizungumza katika uzinduzi huo , Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Borgols, alisema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani, pamoja na maandalizi ya mkutano huo.

“Jeshi la polisi ni wadau wetu muhimu ambao tumekuwa tukishirikiana nao kwa muda mrefu, sisi kama NMB tumefarijika sana kudhamini mkutano huu kwani kutoka katika mkutano huu, mipango na mikakati itakayojadiriwa itakuwa ni manufaa makubwa kwa nchi yetu pamoja na benki ya NMB ambayo matawi yake yote Zaidi ya 170 nchini kote yanapatiwa ulinzi kutoka jeshi la polisi.” Alisema Tom.

Katika maeneo ya ukumbi, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala – huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

Mkutano huo utadumu kwa muda wa siku 5 kuanzia leo Jumatatu tar 26 mpaka ijumaa tarehe 30 Mwezi huu.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Boghols akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani,Mathias Chikawe hundi ya shilingi milioni 75 za udhamini wa Mkutano wa Mwaka wa Maofisa waandamizi wa polisi,ulifunguliwa leo mjini Dodoma na utadumu kwa muda wa siku tano.Kushoto ni Mkuu wa Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa.
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mathias Chikawe (wa pili kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa (kushoto) na Mkuu wa Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu wakiwa kwenye Mkutano wa Mwaka wa Maofisa waandamizi wa polisi,ulifunguliwa leo mjini Dodoma na utadumu kwa muda wa siku tano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Borgols akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Maofisa waandamizi wa polisi,ulifunguliwa leo mjini Dodoma na utadumu kwa muda wa siku tano.
Waziri wa mambo ya ndani ,Mathias Chikawe akizungumza na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Tom Borgols wakati akimpongeza kwa kujitoa kwa hali na mali kudhamini mkutano wa Maafisa wa Jeshi la Polisi unaoendelea mjini Dodoma mara baada ya kutoka ukumbini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad