HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 20, 2014

Mkubwa na Wanawe yasaidia yatima Dar

TAASISI ya Mkubwa na Wanawe Youth Center, imekakabidhi msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha Hisani kilichopo Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam.

Akizungumza jana mara baada ya kukabidhi msaada huo wa vyakula mbalimbali, ikiwemo unga, mchele, maharage, sukari, mafuta ya kula, soda na maji ya kunywa, Mkurugeni wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella, alisema kuwa wamefanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokipata kutoka kwa jamii.

Fella alisema kwa kutambua mchango wa mashabiki huku naye akiwa  yatima, kutokana na kuwapoteza wazazi wake wote, ameona ni muhimu kutoa msaada huo.
 Alisema yeye kwa kushirikiaana na wenzake wameona kila wanapopata nafasi wachangie hata kidogo ili waweze kusaidia.

"Nami kama yatima nina kila sababu ya kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunachangia hata kidogo tunachopata " alisema Fella ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huyo Shinyanga na kuwataka  wasanii na wadau wengine kukumbuka vituo hivyo.

  Naye msanii wa Kundi la Yamoto Band Asilahi Isihaka 'Dogo Aslay'  aliwaomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kwa kusaidia vituo yatima kwa kuwa hawana uwezo, kwa kufanya hivyo inafanya wajisikie faraja.

Naye Mkurugeniz wa kituo hicho, Hidaya Shukrani, aliwashukuru Mkubwa na Wanawe kwa kuwasaidia.

Alisema kuwa msaada uliotolewa ni mkubwa na kuwaomba naomba wengine kujitokeza kuwasaidia kama walivyofanya mkubwa na wanawe.

Alisema katika kituo hicho kina watoto yatima 40 ambao wengine wanasoma na wengine bado watoto wadogohuku kikiwa na changamoto  nyingi kama sehemu maalumu ya kuishi, hivyo mara nyingi kuhamahama na kuomba wadau pamoja na  serikali iwasaidia makazi maalum.
 Mkubwa Fela na wanawe wakitoa misaada kwa watoto yatima kituo cha Temeke jijini Dar es salaam leo kama moja ya shughuli za kusherehekea kutimia kwa mwaka mmoja toka Yamoto Band izaliwe
 Mchele huo
 Mkuu wa kituo akikabidhiwa sehemu ya misaada hiyo na Mkubwa Fela
  Mkubwa Feka na wanawe wakipozi na watoto yatima kituo cha Temeke jijini Dar es salaam leo baada ya kuwakabidhi misaada ikiwa kama moja ya shughuli za kusherehekea kutimia kwa mwaka mmoja toka Yamoto Band izaliwe.
 Misaada
 Mkubwa Feka akiweka sawa sehemu ya misaada hiyo

 Msaada zaidi
 Mkubwa Feka na wanawe wakipozi na watoto yatima kituo cha Temeke jijini Dar es salaam leo baada ya kuwakabidhi misaada ikiwa kama moja ya shughuli za kusherehekea kutimia kwa mwaka mmoja toka Yamoto Band izaliwe
 Mkubwa Feka na wanawe wakipozi na watoto yatima kituo cha Temeke jijini Dar es salaam leo
 Mkubwa Feka na wanawe wakipozi na watoto yatima kituo cha Temeke jijini Dar es salaam leo baada ya kuwakabidhi misaada ikiwa kama moja ya shughuli za kusherehekea kutimia kwa mwaka mmoja toka Yamoto Band izaliwe
 Mkubwa Feka na wanawe wakipozi na mkuu wa  kituo cha yatima Temeke jijini Dar es salaam leo baada ya kuwakabidhi misaada ikiwa kama moja ya shughuli za kusherehekea kutimia kwa mwaka mmoja toka Yamoto Band izaliwe

 Mkubwa Fela na wanawe wakipokea shukurani kutoka kwa mkuu wa kituo
 Mkuu wa kituo akimshukuru Mkubwa Fela na wanae
 Mkuu wa kituo akiwashukuru Yamoto Band
 Mkubwa Fela kituoni hapo
 Vijana wa Yatima Band wakitoa burudani kwa watoto yatima wa Temeke leo
Watoto yatima na majirani wakifurahia burudani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad